Luke 1

1Kwa kuwa watu wengi wamekaa ili kuandika habari za mambo yaliyotukia katikati yetu, 2 akama vile yalivyokabidhiwa kwetu na wale waliokuwa mashahidi walioyaona na watumishi wa Bwana, 3 bmimi nami baada ya kuchunguza kila kitu kwa uangalifu kuanzia mwanzo, niliamua kukuandikia habari za mambo hayo, ewe mtukufu Theofilo, 4 cili upate kujua ukweli kuhusu yale uliyofundishwa.

Kuzaliwa Kwa Yahya Mbatizaji Kwatabiriwa

5 dWakati wa Herode mfalme wa Uyahudi, palikuwa na kuhani mmoja jina lake Zekaria, ambaye alikuwa wa ukoo wa kikuhani wa Abiya. Elizabeti mkewe alikuwa pia mzao wa Haruni. 6 eZekaria na Elizabeti mkewe wote walikuwa watu wanyofu mbele za Mungu, wakizishika amri zote za Bwana na maagizo yote bila lawama. 7Lakini walikuwa hawana watoto, kwa sababu Elizabeti alikuwa tasa; nao wote wawili walikuwa wazee sana.

8 fSiku moja ilipokuwa zamu ya kikundi cha Zekaria, yeye akifanya kazi ya ukuhani Hekaluni mbele za Mungu, 9 galichaguliwa kwa kura kwa kufuata desturi za ukuhani, kuingia Hekaluni mwa Bwana ili kufukiza uvumba. 10 hNao wakati wa kufukiza uvumba ulipowadia, wale wote waliokuwa wamekusanyika ili kuabudu walikuwa nje wakiomba.

11 iNdipo malaika wa Bwana, akiwa amesimama upande wa kuume wa madhabahu ya kufukizia uvumba, akamtokea Zekaria. 12 jZekaria alipomwona huyo malaika, akafadhaika sana, akajawa na hofu. 13 kLakini malaika akamwambia, “Usiogope, Zekaria, kwa maana Mungu amesikia maombi yako. Mkeo Elizabeti atakuzalia mtoto wa kiume, nawe utamwita jina lake Yahya. 14 lYeye atakuwa furaha na shangwe kwako, nao watu wengi watashangilia kwa sababu ya kuzaliwa kwake. 15 mKwa kuwa atakuwa mkuu mbele za Bwana, kamwe hataonja mvinyo wala kinywaji chochote cha kulevya, naye atajazwa Roho Mtakatifu hata kabla ya kuzaliwa kwake. 16 nNaye atawageuza wengi wa wana wa Israeli warudi kwa Bwana Mwenyezi Mungu wao. 17 oNaye atatangulia mbele za Bwana katika roho na nguvu ya Ilya, ili kuigeuza mioyo ya baba kuwaelekea watoto wao, na wasiotii warejee katika hekima ya wenye haki, ili kuliweka tayari taifa lililoandaliwa kwa ajili ya Bwana.”

18 pZekaria akamuuliza malaika, “Jambo hilo linawezekanaje? Mimi ni mzee na mke wangu pia ana umri mkubwa.”

19 qMalaika akamjibu, akamwambia, “Mimi ni Jibraili, nisimamaye mbele za Mungu, nami nimetumwa kwako ili nikuambie habari hizi njema. 20 rBasi sasa kwa kuwa hujaamini maneno yangu ambayo yatatimizwa kwa wakati wake, utakuwa bubu hadi siku ile mambo haya yatakapotukia.”

21Wakati huo watu walikuwa wanamngojea Zekaria nje huku wakishangaa kukawia kwake mle Hekaluni. 22 sAlipotoka akawa hawezi kusema nao, wao wakatambua kuwa ameona maono ndani ya Hekalu. Lakini kwa kuwa alikuwa bubu, akawa anawaashiria kwa mikono.

23 tMuda wake wa kuhudumu Hekaluni ulipomalizika, akarudi nyumbani kwake. 24Baada ya muda usio mrefu, Elizabeti mkewe akapata mimba, naye akajitenga kwa miezi mitano.

25 uAkasema, “Hili ndilo Bwana alilonitendea aliponiangalia kwa upendeleo na kuniondolea aibu yangu mbele ya watu.”

Kuzaliwa Kwa Isa Kwatabiriwa

26 vMwezi wa sita baada ya Elizabeti kupata mimba, Mungu alimtuma malaika Jibraili aende Galilaya katika mji wa Nasiri, 27 wkwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu mmoja jina lake Yusufu wa nyumba ya Daudi. Jina la huyu mwanamwali bikira ni Mariamu. 28 xNaye malaika akaja kwake akamwambia: “Salamu, wewe uliyebarikiwa, Bwana yu pamoja nawe!”

29 yMariamu akafadhaishwa sana na maneno haya, akajiuliza moyoni, “Salamu hii ni ya namna gani?” 30 zNdipo malaika akamwambia, “Usiogope, Mariamu, umepata kibali kwa Mungu. 31 aaTazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanaume na utamwita jina lake Isa. 32 abYeye atakuwa mkuu, naye ataitwa Mwana wa Aliye Juu Sana. Bwana Mwenyezi Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi baba yake. 33 acAtaimiliki nyumba ya Yakobo milele, na ufalme wake hautakuwa na mwisho.”

34Mariamu akamuuliza huyo malaika, “Maadamu mimi ni bikira, jambo hili litawezekanaje?”

35 adMalaika akamjibu, “Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, nazo nguvu zake Yeye Aliye Juu Sana zitakufunika kama kivuli. Kwa hiyo mtoto atakayezaliwa atakuwa mtakatifu, naye ataitwa Mwana wa Mungu. 36 aeTazama, jamaa yako Elizabeti amechukua mimba katika uzee wake, na huu ni mwezi wake wa sita, yeye aliyeitwa tasa. 37 afKwa maana kwa Mungu hakuna lisilowezekana.”

38Mariamu akasema, “Tazama, mimi ni mtumishi wa Bwana. Na iwe kwangu kama ulivyosema.” Kisha malaika akaondoka, akamwacha.

Mariamu Aenda Kumtembelea Elizabeti

39 agWakati huo Mariamu akajiandaa, akaharakisha kwenda katika mji mmoja kwenye vilima vya Uyahudi. 40Akaingia nyumbani kwa Zekaria na kumsalimu Elizabeti. 41 ahNaye Elizabeti aliposikia salamu ya Mariamu, mtoto aliyekuwa tumboni mwake akaruka. Elizabeti akajazwa na Roho Mtakatifu, 42 aiakapaza sauti kwa nguvu akasema, “Umebarikiwa wewe miongoni mwa wanawake, naye mtoto utakayemzaa amebarikiwa. 43 ajLakini ni kwa nini mimi nimepata upendeleo kiasi hiki, hata mama wa Bwana wangu afike kwangu? 44Mara tu niliposikia sauti ya salamu yako, mtoto aliyeko tumboni mwangu aliruka kwa furaha. 45 akAmebarikiwa yeye aliyeamini kwamba lile Bwana alilomwambia litatimizwa.”

Wimbo Wa Mariamu Wa Sifa

46 alNaye Mariamu akasema: “Moyo wangu wamwadhimisha Bwana,

47 amnayo roho yangu inamfurahia
Mungu Mwokozi wangu,

48 ankwa kuwa ameangalia kwa fadhili
unyonge wa mtumishi wake.
Hakika tangu sasa vizazi vyote vitaniita aliyebarikiwa,

49 aokwa maana yeye Mwenye Nguvu
amenitendea mambo ya ajabu:
jina lake ni takatifu.

50 apRehema zake huwaendea wale wamchao,
kutoka kizazi hadi kizazi.

51 aqKwa kuwa ametenda mambo ya ajabu kwa mkono wake;
amewatawanya wale wenye kiburi
ndani ya mioyo yao.

52 arAmewashusha watawala toka kwenye viti vyao vya enzi,
lakini amewainua wanyenyekevu.

53 asAmewashibisha wenye njaa kwa vitu vizuri,
bali matajiri amewafukuza mikono mitupu.

54 atAmemsaidia mtumishi wake Israeli,
kwa kukumbuka ahadi yake ya kumrehemu

55 auIbrahimu na uzao wake milele,
kama alivyowaahidi baba zetu.”

56Mariamu akakaa na Elizabeti karibu miezi mitatu, kisha akarudi nyumbani kwake.

Kuzaliwa Kwa Yahya Mbatizaji

57Ulipowadia wakati wa Elizabeti kujifungua, alizaa mtoto mwanaume. 58 avMajirani zake na jamii zake wakasikia jinsi Bwana alivyomfanyia rehema kuu, nao wakafurahi pamoja naye.

59 awSiku ya nane wakaja kumtahiri mtoto, wakataka yule mtoto aitwe Zekaria, ambalo ndilo jina la baba yake. 60 axLakini mama yake akakataa na kusema, “Hapana! Jina lake ataitwa Yahya.”

61Wakamwambia, “Hakuna mtu yeyote katika jamaa yako mwenye jina kama hilo.”

62 ayBasi wakamfanyia Zekaria baba yake ishara ili kujua kwamba yeye angependa kumpa mtoto jina gani. 63 azAkaomba wampe kibao cha kuandikia na kwa mshangao wa kila mtu akaandika: “Jina lake ni Yahya.” 64 baPapo hapo kinywa chake kikafunguliwa na ulimi wake ukaachiwa, akawa anaongea akimsifu Mungu. 65Majirani wote wakajawa na hofu ya Mungu, na katika nchi yote ya vilima vya Uyahudi watu walikuwa wakinena juu ya mambo haya yote. 66 bbKila aliyesikia habari hizi alishangaa akauliza, “Je, mtoto huyu atakuwa mtu wa namna gani?” Maana mkono wa Bwana ulikuwa pamoja naye.

Unabii Wa Zekaria

67 bcZekaria, baba yake, akajazwa na Roho Mtakatifu, naye akatoa unabii, akisema:
68 bd“Ahimidiwe Bwana, Mungu wa Israeli,
kwa kuwa amewajilia watu wake na kuwakomboa.

69 beNaye ametusimamishia pembe
Pembe hapa inamaanisha nguvu.
ya wokovu
katika nyumba ya Daudi mtumishi wake,

70 bgkama alivyonena kwa vinywa vya manabii
wake watakatifu tangu zamani,

71 bhkwamba atatuokoa kutoka kwa adui zetu,
na kutoka mikononi mwao wote watuchukiao:

72 biili kuonyesha rehema kwa baba zetu
na kukumbuka Agano lake takatifu,
73 bjkiapo alichomwapia baba yetu Ibrahimu:

74 bkkutuokoa kutoka mikononi mwa adui zetu,
tupate kumtumikia yeye pasipo hofu

75 blkatika utakatifu na haki mbele zake,
siku zetu zote.


76 bm“Nawe mtoto wangu, utaitwa nabii wa Aliye Juu Sana;
kwa kuwa utamtangulia Bwana
na kuandaa njia kwa ajili yake,

77 bnkuwajulisha watu wake juu ya wokovu
utakaopatikana kwa kusamehewa dhambi zao,

78 bokwa ajili ya wingi wa rehema za Mungu wetu,
nuru itokayo juu itatuzukia

79 bpili kuwaangazia wale waishio gizani
na katika uvuli wa mauti,
kuiongoza miguu yetu katika njia ya amani.”

80 bqYule mtoto akakua na kuongezeka nguvu katika roho; akaishi nyikani hadi siku ile alipojionyesha hadharani kwa Waisraeli.
Copyright information for SwhKC